Home Sports Business Technology Politics Kids Talk Block Seven

JINA LANGU: UWASE UMWALI

JINA LANGU: UWASE UMWALI

JINA LANGU: UWASE UMWALI

 

Safari yangu katika mchezo wa mpira wa miguu ni kama kupanda milima mirefu isiyo na mwisho. Nilianza kugusa mpira nikiwa msichana mdogo wa shule ya msingi, nikigundua furaha ya kipekee ya kuuchezea mpira—kuuhisi ukizunguka miguuni mwangu na kupata shangwe ya mtoto anayejua kuwa maajabu yanamsubiri mbele.

 

Baada ya kumaliza shule ya msingi, nilianza hatua mpya katika AS Kigali WFC Academy mwaka 2014. Nilikuwa bado mdogo, lakini nikiwa nimejaa hamasa na ndoto kubwa. Nilikaa kwenye academy kwa mwaka mmoja tu, lakini ulikuwa mwaka uliobadilisha maisha yangu. Niliangaza kama radi, na mara moja nikapandishwa hadi kwenye timu ya wakubwa ya AS Kigali WFC.

 

Mwaka 2016, nilikuwa nimekomaa uwanjani kiasi kwamba Rwanda ilinipa nafasi nikaitwa kwenye Timu ya Taifa ya Wanawake ya Wakubwa. Hapo ndipo nilijua safari yangu imeanza kuvuka mipaka ya mahali nilipozaliwa.

 

Niliendelea kuwa shujaa wa AS Kigali hadi nilipojiunga na Fatima WFC, ambako nilicheza misimu miwili (2021–2022 na 2022–2023). Katika misimu yote miwili nilikuwa nahodha, nikisimama mbele ya timu kama rubani anayeongoza ndege katika anga la mashindano makubwa.

 

Baada ya miaka miwili Fatima WFC, nilirudi nyumbani—katika timu iliyonilea—AS Kigali WFC, ambako nilicheza tena misimu miwili (2023–2024 na 2024–2025). Baadaye, niliamua kukabiliana na changamoto mpya na kujiunga na Rayon Sports WFC.

Nilienda Rayon Sports WFC mwezi Julai 2025 kushiriki CAF Women’s Champions League. Baada ya Champions League, tukarudi kupambana kwenye ligi ya ndani katika msimu wa 2025–2026.

Katika mechi tano za mwanzo, nilikuwa tayari nimeshafunga mabao 4 na kutoa pasi za mabao 4. Nyota yangu iliangaza tena mwezi Oktoba nilipotajwa kuwa Mchezaji wa Mwezi, nikipokea tuzo ya mchezaji aliyecheza vizuri zaidi—tuzo iliyothibitisha kuwa safari yangu inaendelea kukua.

 

Ligi bado inaendelea, na safari yangu bado inaendelea kuandikwa—ikiendelea kuelekea kwenye milima mipya inayonisubiri mbele yangu.

Imeandikwa na: MIGISHA Janviére

 

Imetafusiriwa kutoka Kinyarwanda na Jean Marie Shareef

Comments (0)

No comments yet. Be the first to comment!